TANGA DON BOSCO
TECHNICAL SECONDARY SCHOOL
JIMBO KATOLIKI LA TANGA
"Maadili & Elimu Bora"

Manager-0789023719, Taaluma-0753481423,
Mifumo-0626034102.

Uongozi wa Shule
TANGA DON BOSCO

Moral & Quality Education

TANGA DON BOSCO

Moral & Quality Education

TANGA DON BOSCO

Moral & Quality Education

TANGA DON BOSCO

Moral & Quality Education

TANGA DON BOSCO

Moral & Quality Education

TANGA DON BOSCO

Moral & Quality Education

TANGA DON BOSCO

Moral & Quality Education

TANGA DON BOSCO

Moral & Quality Education

Motto wa Shule — Maadili na Elimu Bora

Moral & Quality Education

Elimu bora hujengwa kupitia maarifa, nidhamu, heshima, uwajibikaji, bidii na malezi mema. Tunajenga mazingira yanayomsaidia mwanafunzi kukua kitaaluma, kimaadili na kijamii.

Maadili

Tunasisitiza heshima, uaminifu, uwajibikaji, nidhamu na tabia njema katika maisha ya mwanafunzi.

Elimu Bora

Tunazingatia mazingira yanayomsaidia mwanafunzi kupata maarifa na ujuzi unaohitajika katika maisha na jamii.

Malezi

Malezi bora huenda sambamba na elimu ili mwanafunzi aweze kukua kitaaluma, kimaadili na kijamii.

Maono ya Kizazi

TUNAJENGA KIZAZI CHENYE MAARIFA, MAADILI, NIDHAMU NA UWEZO WA KUTUMIKA KATIKA JAMII.

Historia ya Shule

Historia ya TANGA DON BOSCO TECHNICAL SECONDARY SCHOOL


Shule ya Sekondari ya Ufundi Tanga Don Bosco ni taasisi ya elimu inayomilikiwa na Kanisa Katoliki Jimbo la Tanga chini ya uongozi wa Baba Askofu John Thomas Kiangio.


Awali, taasisi hii ilikuwa ikihudumu kama Chuo cha Ufundi Don Bosco. Hata hivyo, baada ya Kanisa kubaini kuwepo kwa uhitaji mkubwa wa wanafunzi kujiendeleza na masomo ya juu ya ufundi, liliamua kuibadilisha rasmi na kuwa shule ya sekondari ya ufundi.


Shule hii ilipata usajili wake rasmi mwaka 2010 kwa namba ya usajili S.4474 na kuanza udahili wa wanafunzi wake wa kwanza mwaka 2011. Hadi sasa, shule imefanikiwa kutoa wahitimu wa kidato cha nne kwa awamu kumi na tatu.


Chini ya usimamizi madhubuti wa bodi ya shule, taasisi imeendelea kufanya vizuri kitaaluma na kutunukiwa vyeti vya kutambuliwa (Certificates of Recognition) kutoka Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA).


Wakati inaanzishwa, shule ilikuwa na jumla ya wanafunzi 80 na wafanyakazi 9 (walimu 4 na wafanyakazi wasio walimu 5). Kwa sasa, shule ina zaidi ya wanafunzi 500, walimu zaidi ya 20 na wafanyakazi wasio walimu zaidi ya 20.

Aina ya Shule

Aina ya shule na Fani Zitolewazo


TANGA DON BOSCO TECHNICAL SECONDARY SCHOOL ni shule ya sekondari ya mchanganyiko (Wavulana na Wasichana), yenye kidato cha kwanza hadi cha nne tu.


Shule inapokea wanafunzi na wafanyakazi wa imani zote, kutoka mikoa yote Tanzania, na nje ya nchi ya Tanzania. Aidha, shule inafuata mtaala wa elimu wa NECTA, hivyo haifungamani na mitaala mingine kama CAMBRIDGE.


Udahili wa wanafunzi unazingatia ufaulu wa mwanafunzi katika mtihani wetu wa interview ambapo anapaswa kupata wastani wa 65% au zaidi. Ikiwa mwanafunzi amepata nafasi shuleni kwetu kisha baadae akashuka chini ya wastani huu katika mitihani yetu, tunamshauri kutafuta shule nyingine ya kuhamia.


Shule inatoa masomo katika fani zifuatazo:

1. UFUNDI
Masonry and Bricklaying, Technical Drawing, Engineering Science, Computer Application, Life skills, Mathematics, Business Studies, English language, na Historia ya Tanzania na Maadili.


2. SAYANSI
Physics, Chemistry, Biology, Mathematics, Geography, History, Business Studies, Kiswahili, English language, na Historia ya Tanzania na Maadili.

3. SAYANSI YA JAMII
Mathematics, Geography, History, Business Studies, Kiswahili, English language, na Historia ya Tanzania na Maadili.

Falsafa ya Shule

Falsafa ya Shule

Shule inaamini kuwa elimu bora haipaswi kuishia katika kupata alama nzuri pekee, bali inapaswa kumjenga mwanafunzi kuwa mtu mwenye heshima, uwajibikaji, uadilifu na uwezo wa kushirikiana na wengine. Falsafa hii inachagizwa na dira, dhima na motto wa shule.



DIRA YA SHULE (VISION)
"To have Social and Economic Transformation from Poverty to Prosperity."
Tafsiri yake ni "Kuwa na mabadiliko ya kijamii na kiuchumi kutoka kwenye umaskini kwenda kwenye ustawi."

DHIMA YA SHULE (MISSION)
"Training Youths to become self-reliant by providing Education that is centered on solving the needs of our society today."
Tafsiri yake ni "Kuwafundisha vijana kujitegemea kwa kuwapatia elimu inayolenga kutatua mahitaji ya jamii yetu ya leo."

Sheria za Shule

MAKUNDI MATATU YA SHERIA ZA SHULE


1. Sheria ambazo mwanafunzi akivunja atapewa adhabu bila kuandikishwa barua.

(i) Ni lazima kutii kengele inapogongwa kwa ajili ya kuwahi mahali anapotakiwa bila kuchelewa.

(ii) Hakuna ruhusa kwa mwanafunzi kuingia chumba cha walimu (Staff room), maabara, karakana, jiko, computer, nyumba ya walimu au ofisi nyingine shuleni bila idhini ya mhusika.

(iii) Ni lazima kuhudhuria ibada ya pamoja bila ya kutoa kingizio choochote.

(iv) Hairuhusiwi kwa mwanafunzi kuwa na hereni, bangili, pete au mapambo ya aina yoyote.

(v) Hairuhusiwi kwa mwanafunzi kufuga nywele ndefu, kuweka dawa ya nywele, kwa lengo la kuziremba na kufuga kucha.

(vi) Hairuhusiwi mwanafunzi kuvaa nguo zinazobana. Aidha sketi iwe chini ya magoti na upana wa suruali usipungue inchi 16 au sentimita 40.

2. Sheria ambazo mwanafunzi akivunja ataandika maelezo na atapewa adhabu ya kusimamishwa masomo kwa muda (Suspension).

(i) Hairuhusiwi kumiliki au kutumia redio au vifaa vya muziki au kamera za aina yoyote.

(ii) Ni marufuku kumiliki au kutumia visu, sumu, viberiti, mishumaa, petrol na silaha za aina yoyote.

(iii) Ni marufuku kuleta au kuletewa aina yoyote ya chakula au vinywaji shuleni au bwenini. Mwanafunzi anayejiunga na shule hii anawajibika kula chakula kinachoandaliwa na shule bila kisingizio chochote.

(iv) Hairuhusiwi kuzurura ovyo maeneo ya nje ya shule; au mjini wakati unapotoka kwa ruhusa kama vile ruhusa ya matibabu au ibada.

(v) Ni marufuku kuharibu au kupoteza kifaa chochote au mali yoyote ya shule, au ya mtu yeyote shuleni.

(vi) Hairuhusiwi wasichana kwenda kwenye bweni la wavulana na wavulana kwenda kwenye bweni la wasichana.

3. Sheria ambazo mwanafunzi akivunja atafukuzwa shule mara moja, na moja kwa moja.

(i) Ni marufuku kurudia kosa baada ya suspension katika kifungu namba 2 hapo juu.

(ii) Ni marufuku kuiba mali ya mtu yeyote, kwa namna yoyote.

(iii) Ni marufuku kumiliki au kutumia simu au kifaa chochote cha mawasiliano.

(iv) Ni marufuku kujihusisha na uasherati, ulawiti, Ubakaji au usagaji kwa namna yoyote.

(v) Ni marufuku kuhifadhi au kutumia kilevi cha aina yoyote, ikiwemo dawa za kulevya.

(vi) Ni marufuku kujihusisha na kosa lolote la jinai kwa mujibu wa sheria ya nchi.

(vii) Ni marufuku kudharau bendera ya taifa, au picha za viongozi wa serikali.

(viii) Ni marufuku kuoa au kuolewa.

(ix) Ni marufuku kupata mimba, au kusababisha mimba kwa mwanafunzi au mwanamke yoyote; kutoa au kushawishi mtu yeyote kutoa mimba.

(x) Ni marufuku kulala nje ya shule bila idhini ya mkuu wa shule.

(xi) Ni kosa kutohudhuria masomo darasani kwa zaidi ya siku 60 mfululizo.

(xii) Hairuhusiwi kupiga, kupigana; au kutumia lugha chafu au matusi.

(xiii) Ni marufuku kujihusisha na mgomo wa aina yoyote, kuchochea mgomo au kuonyesha dalili yoyote ya mgomo.

(xiv) Ni marufuku kumiliki au kutumia vifaa vya kielektroniki kama vile heater, pasi au tochi ya kuchaji.

(xv)Ni marufuku kuchelewa kuripoti shuleni bila taarifa maalum.

Kuhusu STUDENTS PROGRESS PORTAL

STUDENTS PROGRESS PORTAL (SPP) ni mfumo wa kidijitali wa TANGA DON BOSCO TECHNICAL SECONDARY SCHOOL unaolenga kurahisisha upatikanaji, usimamizi na ufuatiliaji wa taarifa za shule.

Muundo wa Mfumo

Mfumo huu umeundwa kupitia teknolojia za kisasa kwa kutumia lugha mbalimbali za Programming. Kazi hii imefanywa na mtaalam wa utengenezaji wa mifumo ambaye pia ni mwalimu wa Biology na Chemistry katika shule hii.

Aina za Watumiaji

SPP inalenga kutoa huduma kwa watu mbalimbali katika makundi kama vile Mwendesha mfumo (Mkuu wa shule na wataalam wake), Wafanyakazi wote wa shule, wanafunzi wote, wazazi wa wanafunzi, na watu wengine ambao si sehemu ya shule.

Usalama

Mfumo huu unaruhusu kila mtumiaji kuona taarifa zinazomhusu tu katika kundi lake. Mtu asiye sehemu ya taasisi hawezi kuona taarifa za sehemu ya mwanafunzi, mwalimu, au vinginevyo.

Huduma za SPP

SPP inatoa huduma nyingi kwa kila kundi lililoainishwa katika Muundo wa Mfumo hapo juu ikiwemo:

Huduma kwa Watu Wote

Kila mtu (Aliye na asiye mwanajamii wa shule yetu) anaweza kupata huduma zifuatazo Kupitia SPP:
-Kufahamu kuhusu shule, dira, dhima, falsafa, motto na sheria zake
-Kuwafahamu viongozi wa shule na kupata namba zao za simu
-Kuona picha za matukio mbalimbali yanayoendelea shuleni
-Kutuma maoni shuleni, au maombi ya kujiunga na shule
-Kutazama matokeo ya mitihani ya kitaifa ya shule yetu
-Kupata notes za masomo, mitihani, maswali na machapisho mbalimbali

Huduma kwa Wanafunzi

Nje na huduma za watu wote hapo juu, kila mwanafunzi au mzazi anaweza kupata huduma zifuatazo kupitia SPP:
-Kufahamu maendeleo yake katika masomo, na kupata ripoti za matokeo
-Kupata taarifa za michango na matangazo ya shule
-Kuona ratiba ya mambo yote ya kitaaluma yanayoendelea shuleni kila siku
-Kupata majaribio ya masomo mbalimbali mubashara wakati wa likizo (Online Tests)
-Kusasisha picha yake ya wasifu na kubadili nenosiri

Huduma kwa Walimu

Nje na huduma za watu wote hapo juu, kila mwalimu anaweza kupata huduma zifuatazo kupitia SPP:
-Kuona maendeleo ya wanafunzi katika masomo anayofundisha
-Kujaza matokeo ya wanafunzi katika mitihani na majaribio kwa masomo anayofundisha
-Kuona ratiba yake ya vipindi darasani, na ratiba za shughuli nyinginezo.
-Kuandaa maswali au majaribio mubashara (Online Tests)
-Kusasisha picha yake ya wasifu na kubadili nenosiri

Jinsi ya kutumia mfumo

Bonyeza Ingia, weka jina lako la mtumiaji na nenosiri, kisha bonyeza Ingia kwenye Mfumo. Baada ya kuingia, huduma utakazoona zitategemea nafasi na ruhusa zako.

Kuingia kwenye Mfumo

Tumia jina la mtumiaji na nenosiri ulilopewa na shule ili kuingia katika akaunti yako.

Kulinda Akaunti

Linda taarifa zako za kuingia na usimpe mtu mwingine nenosiri la akaunti yako.

Huduma na Ruhusa

Huduma utakazoona ndani ya mfumo hutegemea nafasi yako na ruhusa ulizopewa na shule.

Msaada

Ukiona tatizo au huduma ambayo huna ruhusa nayo, wasiliana na uongozi au msimamizi wa mfumo.

Picha za Shule

Tazama picha mbalimbali zinazoonyesha shughuli, mazingira, wanafunzi na matukio ya TANGA DON BOSCO TECHNICAL SECONDARY SCHOOL.

Mawasiliano ya Shule

Shule inaweza kufikiwa kupitia njia mbalimbali za mawasiliano na eneo lake la shule huko Tanga.

☎

Simu

+255 789 023 719
+255 753 481 423

✉

Barua Pepe

tangadonboscoschool@yahoo.com

⌖

Mahali

Kange, Tanga-Tanzania Tanga, Tanzania.

🚌

Usafiri

Unaweza kufika shuleni kwa usafiri wa umma na binafsi. Ukifika Kange Bus Terminal uliza shule ilipo utaelekezwa.

👤
🔒 👁